Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge amekiri mbele ya Baraza la Maadili kupokea Sh1.6 bilioni kutoka Kampuni ya VIP Enginering and Marketing Limited, zikiwa ni malipo ya kutoa ushauri. Pia, alihoji kama kuna tatizo kutumia taaluma yake ya sheria kuzishauri kampuni binafsi na kujipatia fedha.
Chenge ambaye alitoa utetezi wake jana saa 7:30 mchana, alisema
hakulipwa fedha hizo kwa sababu ni kiongozi wa umma, bali kwa kutoa
ushauri. Alisema aliingia mkataba na kampuni hiyo wa kutoa ushauri wa kisheria
dhidi ya Kampuni ya Mechmer ambazo ni kampuni binafsi zilizokuwa na
mgogoro.
“Nawashangaa mnalalamika Chenge kulipwa na Kampuni ya VIP au wamewafuata na kulalamika kwamba hayakuwa malipo halali,” alihoji.
Alisema hakuna kufungu cha sheria kinachomzuia kutoa ushauri wa kisheria kwa kampuni binafsi. Kuhusu malalamiko kwamba akiwa Mwanasheria wa Serikali aliishauri
kuingia mkataba wa kuuziana umeme kati ya Kampuni ya IPTL na Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO), Chenge alisema anawashangaa wanasheria wa sekretarieti kwa malalamiko hayo.
“Sikuishauri Serikali kuingia
mkataba na IPTL bali ofisi yangu ndiyo iliyotoa ushauri kisheria.
Nakubaliana na walalamikaji kwamba mwaka 1995 nilikuwa mwanasheria wa
Serikali, lakini sikubaliani na madai yao.”
Alisema Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali ilitoa ushauri huo kwa sababu ndiyo jukumu lake.
“Wanasheria ni lazima wafahamu kwamba ile ni taasisi na siyo mtu kama Chenge,” alisema. Alisema ofisi yake ilitoa ushauri wa mikataba mitatu ya IPTL na
Serikali kwa lengo la kuongeza umeme hasa kutokana na ukame uliolikumba
Taifa.
“Naomba baraza lako liyapuuze
kwa dharua zote na kuyatupilia mbali malalamiko ya sekretarieti kwa
sababu hayawezi kukusaidia kutoa uamuzi ulio sahihi,” alisema.
Kuhusu kutumia taarifa alizozipata akiwa mwanasheria wa Serikali na kuzitumia kwa masilahi binafsi, Chenge alisema: “Naomba wachanganue taarifa hizo ni zipi kwa sababu huwezi kumlalamikia mtu kwa jumla lakini kwenye malalamiko husemi. Shahidi wa mlalamikaji, Waziri Kipacha alisema Chenge akiwa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) mwaka 1995, aliishauri Serikali
kuingia mkataba wa miaka 20 na IPTL.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment