Matukio ya uvamizi wa vituo vya polisi yanayokwenda sambamba na
kupora silaha, kuua askari na kujeruhi imebainika kuwa yanasukwa na
baadhi ya watumishi wasiokuwa waaminifu waliopo ndani ya Jeshi la Polisi
au waliofukuzwa kwa makosa mbalimbali ukiwa ni mkakati wa kumdhoofisha
kiutendaji Mkuu wa Jeshi hilo IGP, Ernest Mangu.
Uchunguzi wa kina umebaini kuwa hatua ya baadhi ya askari polisi
kuasi ndani ya jeshi hilo kunatokana na kuchukizwa na mambo kadhaa
yaliyofanywa na IGP Mangu tangu alipoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete
kushika wadhifa huo.
Baadhi ya watumishi wa serikali waliozungumza na gazeti hili kwa
nyakati tofauti walisema mambo ambayo yamechukizwa baadhi ya watu ndani
ya jeshi hilo ni kutokana na kufukuzwa kazi askari wengi na wengine
kubadilishwa vituo vyao vya kazi kwa sababu mbalimbali, mambo ambayo
yamefanyika kipindi cha IGP Mangu.
“Unakumbuka wakati Sanya
(Laurance Sanya) alipokuwa RPC Mbeya kulitokea tukio moja la uvamizi wa
Kituo cha Polisi Tunduma lakini kipindi cha utawala wa IGP Mangu
yamejitokeza mengi hapa kuna sababu,” alisema.
Alisema IGP Mangu amekuwa mkuu wa Jeshi la Polisi ambaye ameongoza
kufukuza askari hususani wanaokula rushwa ambao hakuwavumilia na ndiyo
hao hao wamegeuka kuwa adui wa jeshi hilo kwa kushirikiana na jamaa na
ndugu zao ambao bado wapo ndani ya utumishi wa jeshi hilo.
Jambo la pili lililojenga hasira kwa askari hao ni hatua ya IGP Mangu
kutoa tishio kwamba askari wote ambao wana vyeti vya kughushi
wajisalimishe.
“Taarifa za Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inaonyesha kuwa zaidi ya watumishi 10,000
wa Jeshi la Polisi wana vyeti vya kughushi lakini kwa bahati mbaya
katika awamu zote za utawala wahusika wamekuwa wakiachwa bila
kuchukuliwa hatua na sasa IGP Mangu amekuja kuyavumbua,” kilisema chanzo kutoka ndani ya serikali.
Chanzo hicho kilieleza kuwa baada ya IGP Mangu kutoa tamko la kutaka
watumishi ndani ya jeshi hilo wenye vyeti vya kughushi wajisalimishe
ndipo matukio ya uvamizi wa vituo vya polisi yalipoibuka kwa kasi ili
mkuu huyo wa Jeshi la Polisi aonekane ameshindwa kazi na kufukuzwa.
Anaeleza kuwa kuhusisha matukio ya uvamizi huo na suala la ugaidi
inaweza kuwa siyo kweli kwa asilimia kubwa kwa sababu mara nyingi
magaidi wanaofanya matukio makubwa mfano nchi jirani wanakuwa na silaha
kubwa kama AK-47 sasa inawezekanaje kama kweli ni magaidi hapa kwetu
wawe wanapora bunduki ndogo za SMG.
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Hellen Kijobisimba, alisema matukio ya uvamizi wa vituo vya polisi yameanza kujitengeneza pole pole na sasa yamekuwa makubwa.
Alisema wakati hali ya kiuslama ikibadilika, Jeshi la Polisi kwa
upande wake bado halijabadilika ili kukabiliana na matukio hayo.
“Zamani usingeweza kuona askari
anayetembea barabara ananyang’anywa silaha hata kama huyo askari
yukoje, lakini hivi sasa polisi wapo kwenye doria wanavamia na
kunyanng’anywa silaha, wanaenda kama vile nyumbani kwao na bahati mbaya
polisi wenyewe hawajashtuka,” alisema.
Kijobisimba alisema polisi wangekuwa wamebadilika kiutendaji matukio hayo yasingetokea. Alisema sababu nyingine ya kuibuka kwa matukio hayo ni ndani ya Jeshi
la Polisi lenyewe kuna tatizo ambalo inabidi litafutiwe ufumbuzi.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment