Katika hoteli ya Serena akiwa na walinzi wake 7, amefika na kuamua kuweka kila kitu wazi kuhusu ukimya wake. Soma hapo chini alichozungumza
Slaa: Kila mtu ana kiu ya kusikia Dr Slaa anasema nini, sijawahi kuona waandishi wengi hivi
Slaa: Wengi mnafahamu sina tabia ya kuyumbishwa, ninasimami a lile ninaloamini, ijulikane kama binadamu sina chuki na mtu
Slaa: Mimi sikuwa likizo kama mlivyoambiwa na wengine. Nimeamua kuachana na siasa tarehe 28 Julai 2015 saa 3 usiku.
Naomba ijulikane kuwa nilishiriki majadiliano ya awali juu ya ujio wa Lowassa ndani ya CHADEMA, ila sikuafiki ujio wake.
Slaa: Mchakato ndani ya CHADEMA ulianza mapema na jina langu lilipitishwa lakini bado sikuitangaza popote.
Slaa: Suala la Msingi ni kuangalia kama ni ASSET au LIABILITY, ASSET kwa maana kwamba anakuja na watu wangapi kwenye chama
Slaa: Tuliambia anakuja na wabunge wanaomaliza muda wao zaidi ya 50 na viongozi wengine toka CCM.
Slaa: Siku zikapita sikupewa majina ya wabunge hao, wenyeviti wa CCM mikoa wala makatibu wakuu.
Slaa: Upotoshwaji kwamba Dr Slaa alikubali toka mwanzo si kweli naomba viongozi wangu waseme kweli.
Slaa: Kamati kuu tumekaa toka saa 9 hadi 12:30 kikao kikavunjika, ikasemwa iundwe kamati ndogo kunishawishi, nikakataa.
Slaa: Niliandika barua ya kujizuru ndani ya kamati kuu kwa mwenyekiti wakati huo akiwa Profesa Safari, ambaye aliichana.
Post a Comment