Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema kuwa haoni tatizo lolote wala hashangai kusikia mgombea huyo akiikosoa serikali yake kwa kuwa Tanzania inahitaji muelekeo mpya.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo mjini Washington, Marekani aliopokuwa akiongea na wafanyakazi wa Taasisi ya NDI yenye uhusiano na Chama Cha Republican, IFES na United States Institute of Peace (USIP).
Alisema kuwa alifuatwa na watu mbalimbali wakimueleza kuhusu kauli za Dk. Magufuli kwenye majukwaa ya kampeni lakini aliwaambia kuwa jambo hilo ni sahihi na jema.
“Niliwaambia nchi yetu inahitaji mawazo mapya na mwelekeo mpya ulio tofauti na uongozi wangu. Niliwaambia tusiporuhusu jambo hilo kufanyika, nchi yetu itabakia pale pale ambapo nimeifikisha mimi,” alisema Rais Kikwete.
“Haya yatakuwa ni makosa makubwa sana kwa sababu nchi yetu lazima isonge mbele kwa mawazo mapya na staili mpya ya uongozi,” aliongeza.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment