Mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na
vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Edward
Lowassa amesema kama atachaguliwa atahakikisha anafuta kodi ambazo
zimekuwa mzigo kwa wananchi wa kipato cha chini.
Wakati upepo wa kisiasa ukizidi kubadilika na huku kadi namba 8 ya
CCM ikiwa tayari imekwisha kurejeshwa Dar es Salaam, Mgombea wa urais wa
Edward Lowassa anasema kama watanzania watampatia ridhaa ya kuwa rais
wa nchi atahakikisha kila mtanzania ananufaika na keki ya taifa akianzia
na wafanaykazi wa kada ya chini.
Uwepo wa kodi mizigo kwa watanzania wanyonge ni tatizo ambalo
serikali yake italishughulikia ndani ya siku 100 za kwanza ikiwa ni
pamoja na kuboresha huduma za jamii hasa katika vituo vya kutolea huduma
za afya.
Akihutubia maelf ya wakazi mjini hanang ambapo amekuwa mbunge kwa
zaidi ya miaka 20, Fredrick Sumaye amewataka wanahanang na watanzania
kwa ujumla kutokuhadaika na ahadi butu za CCM, kwani uongozi huo wa CCM
ndio umechochea umasikini uliokithiri kwa watanzania.
Huku akitumia usafiri wa chopa amefanikiwa kuhutubia mikutano
katika maeneo ya Dogobeshi, Magugu, kabla ya kuhitimisha kwa kuhutubia
maelf ya wakazi wa jimbo la Hanang mkoan Manyara katika uwanja wa
makondeko.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment