Tume ya taifa ya uchaguzi imeanza
kusambaza mikoani mfano wa fomu zitakazotumika katika kupiga kura kwenye
uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwezi huu huku ikiwataka wagombea
wa nafasi za Udiwani, Ubunge na urais kuzihakiki fomu hizo.
Mkurugenzi wa ugavi na manunuzi wa tume hiyo Elikoi Njaila amesema
kinachotakiwa kufanyika sasa ni wagombea kuangalia kama zina dosari
yoyote ili ziweze kurekebishwa kabla ya kutolewa za mwisho
zitakazotumika katika upigaji huo wa kura.
ITV imefika kwa mmoja kati ya wagombea urais Bw.Fahmi Dovutwa wa
chama cha UPDP ambaye amesema kuwa fomu ya mgombea urais ipo katika hali
stahili na imekidhi mambo yote ambayo wagombea urais walihitaji yawepo
katika fomu hizo.
Post a Comment