Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MADUKA YA UCHUMI KUFUNGWA TANZANIA NA UGANDA

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.

Maduka ya jumla ya Uchumi yametangaza kufungwa kwa oparesheni zake nchini Tanzania na Uganda katika zoezi la kubana matumizi.

Mkurugenzi mkuu wa maduka hayo Dr.Julius Kipng'etich amesema kuwa bodi yake imeamua kufunga vituo hivyo kwa lengo la kutathmini muundo wa oparesheni zake nchini Kenya.

''Maduka yetu nchini Tanzania na Uganda yanajumlisha asilimia 4.75 ya oparesheni zetu licha ya kutugharimu asilimia 25 ya oparesheni zetu''.

Maduka ya uchumi katika mataifa hayo mawili hayajazalisha faida yoyote katika kipindi cha miaka 5 swala ambalo linalazimu faida zinazopatikana katika maduka ya Kenya kutumika,alisema Kipng'etich.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa tayari maduka hayo yameandika barua kwa Mamlaka ya masoko nchini Kenya,

soko la hisa pamoja na washikadau muhimu kuhusu uamuzi huo na kuongezea kwamba hivi karibuni uchumi itahitaji kuungwa mkono na wamiliki wa hisa ili kuidhinisha mpango huo.

Maduka yote katika mataifa hayo mawili yamefungwa.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top