Jeshi la polisi Mkoa wa Mtwara limesema linachunguza kwa kina taarifa za kutekwa kwa mgombea
Jeshi la polisi Mkoa wa Mtwara limesema linachunguza kwa kina taarifa za kutekwa kwa mgombea ubunge jimbo la Mtwara mjini (Chadema) Joel Nanauka na endapo litabaini kuna udanganyifu ameufanya dhidi ya tukio hilo hatua za kisheria zitachukuliuwa dhidi yake.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya mgombea huyo kutoweka nyumbani kwao eneo la Coco Beach mjini Mtwara majira ya saa 12 jioni siku ya Jumatatu na simu zake zikionyesha kufungwa baada ya kutoweka kwake.
Akizungumza leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe alisema wanalichunguza tukio hilo ili kubaini kama kuna ukweli, kutokana na kuwapo kwa tetesi zinazoonyesha huenda tukio hilo lilipangwa kutokana na mazingira ya kutoweka kwake hadi kupatikana.
“Jana majira ya saa 7 tulipata taarifa za mgombea wa ubunge Chadema kuwa amepotea toka alipoagana na familia yake kwenda eneo la Mnarani kuonana na jamaa zake na hakuonekana tena, hadi leo amepatikana akiwa katika hali ambayo sio nzuri sana na yuko hospitali anaendelea na huduma lakini tutaendelea kuchunguza kujua ni kitu gani kilitokea,”alisema Kamanda Mwaibame
Post a Comment