Uturuki imesema kwamba ilituma ndege zake mbili za kijeshi aina ya F-16
kuzuia ndege ya kijeshi ya Urusi iliyokuwa imeingia katika anga yake
bila ruhusa Jumamosi.
Ndege hiyo ya Urusi “iliondoka anga ya Uturuki na kuingia” Syria baada ya kuzuiwa, wizara ya mashauri ya kigeni ya Uturuki imesema.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uturuki amezungumza na mwenzake wa Urusi, pamoja na mawaziri wengine kutoka kwa shirika la kujihami la Nato.
Uturuki imesema ilizuia ndege hiyo ya Urusi katika eneo lililo kusini mwa jimbo la Yayladagi/Hatay.
Wizara ya mashauri ya kigeni mjini Ankara ilimwita balozi wa Urusi nchini humo “kulalamika vikali” kuhusu kisa hicho.
Russia imekuwa ikitekeleza mashambulio ya kutoka angani nchini Syria dhidi ya wapinzani wa Rais Bashar al-Assad.
Mashambulio hayo yalinaza Jumatano wiki iliyopita, Urusi ikisisitiza kwamba inalenga tu maneoe yanayodhibitiwa na Islamic State (IS). Lakini wanaharakati wa kutetea haki nchini Syria wanasema ndege za Urusi pia zilishambulia makundi mengine yanayompinga Rais Assad.
Wiki iliyopita, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alitaja hatua ya Urusi kuingilia mzozo nchini Syria kama “kosa kubwa” ambalo litapelekea kutengwa Zaidi kwa Moscow.
Post a Comment