Wametuletea hii mpya ya gari la mizigo linaloweza kujiongoza lenyewe.
Imetokea
kwenye jimbo la Nevada Marekani ambako Freightliner walipewa kibali cha
kulifanyia majaribio gari la mizigo ambalo lina uwezo wa kujiongoza
lenyewe na kumpa dereva nafasi ya kupumua kidogo.
Tofauti na magari mengine ambayo yanaweza
kujiendesha yenyewe, hili ni lazima dereva awepo pembeni kama kawaida
ila akishaliruhusu kujiendesha lenyewe anaweza kuendelea na kazi zake za
pembeni kama kupanga safari zijazo na mengine ya kawaida lakini anakua
macho kwa kinachoendelea barabarani kama inavyoonekana kwenye picha ya
kwanza.
Ni gari ambalo linaweza kujiongoza kwa msaada wa Radar sensors and cameras ambapo
japo hawajasema muda kamili wa gari hili kuanza kufanya kazi,
imeripotiwa kwamba haitachukua muda mrefu kuingia barabarani.
Freightliner inamilikiwa na Daimler AG ambao pia ndio wanahusika kutengeneza magari ya kifahari ya Mercedes-Benz
Post a Comment