Wakati
wa muda wa kuelekea nyumbani watu hulazimika kupigania viti vichache
vilivyopo huku wengine wakilzimika kutumia njia nyengine kuingia vyombo
hivyo vya usafiri.
Mabasi hayo yanayojulikana kama Dala Dala yalianza
oparesheni zake miaka ya 70 ili kukabiliana na swala nyeti la ukosefu wa
magari ya uchukuzi.
Wakati huo safari fupi iligharimu shilingi 5
za Tanzania ambazo zilikuwa sawa na dola moja na hivyobasi kuanza kwa
jina la Dala Dala.
Kwa sasa safari fupi hugharimu shilingi 500 za Tanzania ambapo ni robo ya dola moja. Lakini bado abiria wanalalama kwamba wangetaka usafiri ambao ni rahisi na wenye kustarehesha.
Wanasema kuwa hilo ni swala nyeti ambalo linafaa kupewa kipaumbele na serikali inayotarajiwa.
Madereva vilevile hulalamikia bei ya juu ya mafuta ya petroli pamoja na kodi za kiwango cha juu zinazotozwa na mamlaka.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment