Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Yanga SC leo wameuanza tena upya utaratibu wao wa kutoa dozi kubwa baada ya leo kuifunga Toto African ya mwanza goli 4-1 katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katika mchezo wa leo ambao umeshuhudia beki kutoka Togo Bossue akicheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya vodacom Yanga waliuwanza mchezo kwa kasi ya kawaida.
Katika dakika ya kwanza ya mchezo shuti la Amisi Tambwe amanusura iliandikie yanga goli la kuongozi ambapo shuti lake lilipaa.
Toto African wakicheza muda mwingi katika eneo lao na kukosa ubunivu wanapovuka nusu ya upande walishuhudia nyavu zao zikitingiswa na Juma Abdul katika dakika ya 8 akiunga mpira wa kona fupi iliyopigwa na Haruna Niyonzima.
Kuingia kwa goli hilo kulipunguza kasi ya yanga katika mchezo huo na kupelekea Toto African kuaza kuonana na kujaribu kufika katika eneo la yanga lakini wakikosa ubunifu wa kupenya safu ya ulinzi ya yanga iliyokuwa chini ya Bosue.
Mwishoni mwa kipindi cha kwanza yanga walipata penati ambayo ilipigwa na Donald Ngoma na kipa wa Toto African akaicheza penati hiyo na kupelekea yanga kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.
Katika kipindi cha pili Yanga walianza kwa mabadiliko ambapo Saimon Msuva aliingia kuchukuwa nafasi ya Juma Abdul, kitendo kilicho rejesha kasi ya yanga.
Mpira wake wa kwanza kuugusa Msuva nusura aindikie yanga goli la pili katika dakika ya 46 kabla ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa Thaban Kamusoko na kuiandikia Yanga goli la pili katika dakika ya 48.
Toto African nao waliandika goli lao pekee katika dakika ya 56 kupitia kwa Miraji Adam, ambapo alimalizia kwa kichwa mpira uliotemwa na Ally Mustapha.
Kuingia kwa goli hilo kuliamsha kasi ya yanga na kutengeneza nafasi mbili ambazo walishindwa kuzitumia kabla ya Amisi Tambe kuiandika yanga goli la tatu katika dakika ya 80.
Katika dakika ya 89 Msuva alihitimisha karamu ya magoli kwa yanga akiunga pasi murua ya Andrey Countinho aliyeingia kuchukuwa nafasi ya Geofrey Mwashuiya na kuipa yanga ushindi wa goli 4-1 mbele ya Toto Africans.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.
Share habari hii na wenzio wajue
Post a Comment