Kwa kawaida mwanamke anapopata ujauzito huanza kuhisi hali ya tofauti mwilini mwake jabo baadhi ya wanawake huwa ni ngumu kwao kufahamu dalili hizo za ujauzito.
Kuna dalili za awali kabisa ambazo huashiria ujauzito kwa mwanamke na miongoni mwa hizo ni kama zifuatazo.
Kuhisi maumivu kwenye matiti, hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka pale ambapo yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huchangia kuongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa tofauti na ilivyo kawaida.
Kuhisi maumivu mwilini, mwanamke mwenye dalili za ujauzito huanza kuhisi maumivu kama vile unataka kuingia katika siku zako.
Kuchoka, mama mjamzito huweza kuhisi kuchoka sana na kutokuwa na hamu ya kufanya chochote na kuhitaji kulala tu. Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na usingizi.
Dalili nyingine za awali ni pamoja na chuchu kuwa nyeusi, lakini baadhi ya wanawake ambao ni weuzi huwa ni ngumu kwao kuona dalili hii.
Kichefuchefu, hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wote ambao hupata ujauzito, ambapo wengi wao hujikuta wakihisi kichefuchefu na kutapika nyakati za asubuhi.
Mbali na hayo dalili nyingine za awali wakati wa ujauzito ni kwenda haja ndogo mara kwa mara, miguu kuvimba, kuumwa kichwa japo si mara zote na hata kukosa choo pia.
Post a Comment