Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
Juzi nimefungua uzi wenye kichwa cha habari, "USHUHUDA: Jinsi kampuni za mafuta zinavyokwepa ushuru" nikatoa mfano mmoja wa kampuni ya OILCOM inavyokwepa ushuru. Kuna watu wameni-inbox vitisho.
Sasa natoa mfano mwingine wa OILCOM hiyohiyo.
Baada ya gas ya songosongo kuanza kuchakatwa (Gas processing). Kampuni ya OILCOM ilipata tender ya kununua Naptha ambayo ni byproduct ya gas processing. Hii naptha ni mojawapo ya condensate katika Natural Gas Liquids (NGL) ambazo huwa zina-liquify katika surface separator.
Kwa wasioijua hii Naptha ni ile thinner inayotumika kuchanganyia rangi. Sasa hii naptha inatumika katika viwandani kutengenezea Rangi. Sasa OILCOM ndio Dealer mkubwa wa hiyo naptha pale songosongo.
Huwa anapeleka meli pale Songosongo na kupakia mzigo wa kutosha na kuja kuushusha kwenye depot yake pale kurasini. Kwa mkataba wake OILCOM ni kwamba anaiuza kwenye viwanda vya rangi vya hapa nchini na nyingine ana-export nje ya nchi.
Anachokifanya kwenye depot yake pale kurasini ni kui-blend na Petrol (PMS) kwa ratio nzuri na kuongeza na Octane boosters ili afikie viwango vinavyohitajika vya AKI (Anti Knocking Index) na anatuuzia kwenye service station zake kama petrol.
Parameter anayoi-monitor kwenye hii petrol anayotu-blendia ni hiyo OCTANE number tu kwa sababu anajua kuwa akikosea hiyo atauwa injini za magari yote yanayotumia petrol na effect yake watu wataiona immediately wakijaza kwenye station zake.
Parameter nyingine kama oxygen content na vapour pressure hashuguliki nazo kwakuwa effect zake zipo kwenye ulaji wa mafuta wa injini na kutoa moshi. (Effects of low and high oxygen content)
Hii petrol yenye naptha ya songosongo tumeuziwa kwa muda mrefu sana na wakuu wanajua kuanzia EWURA hadi TRA.
Yupo afisa mmoja wa TRA wa kitengo cha mafuta ambaye alikuwa ndio kama Resident Custom Officer pale Oilcom anaitwa GEORGE, yeye ndio alikuwa kiunganishi wa OILCOM kwenye haya magumashi.
Source:Jamii Forum
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.
Share habari hii na wenzio wajue
Post a Comment