Moto wateketeza jengo la posta eneo la soko la sabasaba manispaa ya Dodoma.
Moto mkubwa umezuka na kuteketeza jengo la posta ndogo lililopo eneo la soko la sabasaba manispaa ya Dodoma huku vitu nyote viliyokuweno ndani ya jengo hilo vikiungua ambapo gharama halisi na hasara ikishindwa kufahamika mara moja.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ya moto wanadai chanzo ni hitilafu ya umeme iliyojitokeza katika jengo hilo na kusababisha baadhi ya maeneo kushika moto ambao ulisambaa kwa kasi na kuteketeza mali na thamani zilizokuwemo ndani yake.
Akizungumzia ajali hiyo meneja wa posta mkoa wa Dodoma Magreth Ulyomi amesema alipata taarifa kutoka kwa mmoja kati ya wafanyakazi wa ofisi hyo kuwa kuna cheche za moto zinaonekana katika jengo hilo kabla ya kuwaka na kuteketea.
Awali muda mfupi baada ya kuzuka kwa moto huo jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Dodoma lilifika lakini lilishindwa kuingia kwenye eneo la tukio kutokana na ujenzi holela wa vibanda vya wafanyabiashara sokoni hapo hali iliyochangia mapambano dhidi ya moto huo kushindwa kufanyika kwa ufanisi.
Post a Comment