Makamu wa rais Mh.Samia Suluhu azindua mpango wa kutoa mafunzo ya uongozi kwa wanawake DSM.
Makamu wa rais, Mh Samia Suluhu Hassan, ameyataka mashirika mbalimbali nchini hasa sekta binafsi kuwaingiza wanawake kwenye bodi ili kukuza uchumi, kuongeza kipato cha wananchi na kuondokana na umasikini.
Mh Samia ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mpango wa kutoa mafunzo ya uongozi kwa wanawake, namna ya kufanya kazi, kuongoza nafasi za ukurugenzi na bodi mbalimbali, ulioandaliwa na chama cha waajiri Tanzania ATE.
Waziri wa sera, bunge, kazi, vijana, ajira na walemavu Mh Jenista Mhagama akizungumza katika uzinduzi huo amesema asilimia kubwa ya nguvu kazi iko sekta isiyo rasmi hivyo ameitaka ATE kufikiria namna ya kugawa huo mpango kusaidia wanawake ngazi ya chini.
Kwa upande wake, mkurugenzi mtendaji wa ATE Dk Aggrey Mlimuka na Mwenyekiti wa ATE Afrika Almas Maige amesema mpango huo utawezesha wanawake kupata mafunzo ya namna ya kusaidia kuwa wakurugenzi wa bodi na kuingia kwenye nafasi za kufanya maamuzi makubwa na yataanza kutolewa kwa walimu.
Post a Comment