Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
Baada ya mjadala wa jana bungeni juu ya matumizi ya "Bangi na mirungi" ulioibuliwa na Mbunge wa Geita Vijiini Joseph Kasheku Musukuma, nilimtafuta daktari Chriss Cyrilo (MD) aeleze kama bangi ina faida kama alivyosema Msukuma au ina hasara. Na haya ndio maelezo ya daktari.
____________________________________
FAIDA 11 ZA KIAFYA ZA MATUMIZI YA BANGI (MARIJUANA).
Na Dr.Christopher Cyrilo (MD)
UTANGULIZI;
Katika baadhi ya nchi Duniani, matumizi ya bangi yamehalalishwa kuzingatia utashi wa mamlaka za nchi husika. Uruguy na Marekani (katika majimbo 20) ni mifano ya nchi hizo. Tafiti mbalimbali za kiafya zimefanyika na kupelekea ugunduzi kuwa bangi huweza kutumika kama tiba kwa baadhi ya magonjwa, isipokuwa haipaswi kutumika ovyo kama ilivyo kwa dawa zingine.
Zifuatazo ni faida 11 za kiafya za bangi. Kisha tutaeleza na athari hasi za bangi hapo baadae.
1. Inaweza kutumika kukinga na kutibu presha ya jicho (glaucoma), bangi inapunguza presha ya jicho (intraocular pressure) kwa watu wenye presha ya kawaida na hata wale ambao presha ya jicho iko juu( glaucoma).
2. Inaweza kuboresha afya ya mapafu na kupunguza athari za tumbaku katika mapafu. Januari 2012, tafiti zilionesha bangi haiathiri kazi za mapafu badala yake huongeza ufanisi wa mapafu.
3. Huweza kuzuia kifafa. Kemikali aina ya "Tetrahydrocannabinol" au "THC" iliyopo katika bangi huambatana na seli za ubongo zinazochochea umeme katika mfumo wa fahamu. Muambatano huo hupunguza msisimko (excitability) wa mfumo wa fahamu na kuzuia kutokea kwa kifafa.
4. Kuzuia kuenea kwa baadhi ya kansa, "Cannabidiol au CBD" ni kemikali iliyopo kwenye bangi ambayo hupunguza kuenea kwa kansa mwilini. Mfano, kansa ya matiti.
5. Inapunguza wasiwasi, maumivu na kichefuchefu, hata hivyo ikitumiwa kwa kiasi kikubwa huweza kuongeza wasiwasi.
6. Hupunguza na kutibu matatizo ya kutetemeka kwa misuli, (Parkinsonism)
7. Bangi huweza kutibu magonjwa ya utumbo (Inflammatory bowel diseases). Mwaka 2010 katika chuo cha Nottingham, tafiti ziligundua kuwa kemikali zilizopo kwenye bangi husaidiana na seli za mwilini kuongeza kinga za mwili na ufanisi wa utumbo.
8. Kupunguza maumivu ya viungo. Bangi hupunguza maumivu, hupunguza miwasho na kuleta usingizi.
9. Huboresha ngozi na kuchangamsha kazi za mwilini, Pia huongeza matumizi ya sukari mwilini.
10. Huongeza uwezo wa kubuni vitu (creativity), uwezo wa kukumbuka na uwezo wa kuzungumza.
11. Huweza kusaidia watu wanaopata matatizo ya mfadhaiko kutokana na kumbukumbu za mambo ya kutisha (post traumatic stress disorder) Mfano, Kwa wahanga wa majanga ya asili na yale yasio ya asili kama vita, moto, tsunami nk. Watu hao hupata kuona upya matukio ya kutisha walioshuhudia zamani na huweza pia kuyaona katika ndoto. Bangi huweza kuwasaidia kuepuka tatizo hilo. Maveterani wa vita ni mfano mzuri kabisa.
ANGALIZO. Matumizi ya kiafya ya bangi yanapaswa kuwa chini ya maelekezo ya daktari au mtaalamu wa afya, kwa sababu athari zake hutegemea kiasi cha matumizi na hali ya afya ya mtumiaji. Inaaminika kuwa Bangi ina athari chache kulinganisha na pombe.
Dr.Chriss Cyrilo (MD).
Asante.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.
Share habari hii na wenzio wajue
Post a Comment