Polisi waanza mpango wa matokeo makubwa kwa kuhakikisha usalama wa raia.
Wizara ya mambo ya ndani kupitia jeshi la polisi wameanzisha mpango maaalum wa kuhakisha usalama wa raia na mali zao unaimarika ambapo waziri Mh Charles Kitwanga amemwagiza mkuu wa jeshi la polisi nchini Ernest Mangu kuhakikisha kuwa mpango huo unatekeleza kama ulivyopangwa lengo likiwa ni kuona matukio ya kihalifu yanapungua kama siyo kuisha kabisa.
Mh Kitwanga ametoa agizo hilo muda mfupi baada ya kusaini mkataba wa makubaliano baina ya waziri Kitwanga na IGP Mangu kuwa jeshi la polisi litatekeleza mpango huo ambao unaratibiwa kupitia mradi wa matokeo makubwa sasa.
Naye kamanda IGP amesema wamejipanga vyema kuhakisha kuwa wanatekeleza mpango huo na kwa kuanza wataanza na wilaya ya Kinondoni kwa sababu ndio inayongoza kwa matukio ya kihalifu.
Kwa upande wake afisa mtendaji mkuu wa BRN Bw Omari Isa amesema kabla ya kupatikana kwa mpango huo maafisa wa polisi na viongozi mbalimbali wa serikali za mitaa walikaa chini na kukubaliana ni mambo gani ya msingi ambayo watatakiwa kuyafanyia kazi na ni kwa namna gani.
Post a Comment