Watumishi 4 wa hospitali ya mkoa wa Mwanza wasimamishwa kazi kwa tuhuma za rushwa.
Watumishi wanne katika hospitali ya rufaa mkoa wa Mwanza Sekou Toure wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kujihusisha na mianya ya rushwa wakati wa utoaji huduma, biashara haramu ya damu salama inayouzwa kwa magendo kati ya shilingi 45,000 kwa yuniti moja hali inayosababisha wagonjwa kukosa huduma inayositahili kwa wakati.
Huyo ni katibu wa afya katika hospitali ya rufaa mkoa wa Mwanza Sekou Toure Bw.Danny Temba akizungumza na ITV katika mahojiano maarumu juu ya utoaji huduma za afya kwa jamii ambapo amebainisha maeneo yaliyokithiri kwa rushwa katika utoaji huduma za afya ambapo mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dkt Rwakyendela Onesmo akitoa angalizo kwa watumishi watakaobainika wakijihusisha na mianya ya rushwa.
Hatua ya kusimamishwa kazi watumishi wanne kwa tuhuma za rushwa imetokana na malalamiko ya wananchi juu ya huduma duni inayotolewa katika hopitali ya rafaa mkoa wa Mwanza Sekou Toure ambapo wodi ya mtoto wanalazimika kulala watu wanne katika kitanda kimoja yani mama wawili na watoto wawili kama wanavyobainisha wagonjwa.
Akijibu malalamiko hayo mganga mfawidhi hospitali ya rufaa mkoa wa Mwanza Sekou Toure Dkt Bahati Msaki amekili kuwepo kwa changamoto ambazo zinasababishwa na ongezeko la wagonjwa na bajeti ndogo inayotolewa na serikali ya shilingi milioni 143 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na kwamba zaidi ya shilingi bilioni 34 zinahitajika kujenga miundombinu mbalimbali katika hospitali hiyo.
Post a Comment