Serikali ya Uingereza yarizishwa na utendaji kazi wa rais wa Tanzania Dkt. Magufuli.
Serikali ya Uingereza imeeleza kuridhishwa na utendaji kazi wa rais wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli katika kubana matumizi pia kupambana na rushwa na kwamba nchi yake iko tayari kutoa ushirikiano kwa Tanzania katika kuliimarisha jeshi la polisi na idara ya mahakama.
Hayo yamesemwa na balozi wa Uingereza hapa nchini Dianna Melrose alipokutana na kufanya mazungumzo na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon anaridhishwa na hatua zinazochukuliwa na rais John Pombe Magufuli katika kupambana na rushwa hapa nchini.
Mbali na balozi huyo wa uingereza hapa nchini pia rais Dkt John Pombe Magufuli pia amekutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Afrika Kusini hapa nchini Thamsanqa Mseleku, na kisha Mh Mohamed Yasserel Shawaf balozi wa Misri hapa nchini mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katika tukio jingine rais Dkt John Pombe Magufuli amepokea hati za utambulisho za mabalozi ambapo balozi wa kwanza kuwasili Ikulu na kukabidhi hati zake ni balozi wa jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC Mh Jean Pierre tshampanga na kisha kufuatiwa na balozi wa Namibia Mh Theresia Samaria matukio yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Aidha, rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
Post a Comment