Tamisemi yawataka watendaji mkoani Arusha kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Naibu waziri wa Tamisemi Bw.Suleimani Jaffo amemtaka katibu tawala wa mkoa wa Arusha kumpatia orodha ya watendaji wanaoendelea kufanya kazi kwa mazoea na kusababisha wananchi kuteseka bila sababu za msingi ili hatua zikiwemo za kuwafukuza kazi zichukuliwe haraka kwani wakati wa kubembelezana umekwisha.
Mh.Jaffo ameyasema hayo baada ya kupewa taarifa inayopingana na hali halisi ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali likiwemo la kushughulikia maafa yanayowapata wananchi iliyosababisha baadhi ya watendaji kushindwa kujieleza na wengine kutupiana lawama na kuikana maelezo yao wenyewe. Soma zaidi habari hii kupitia kwenye link iliyopo==>> HAPA
Post a Comment