Wabunge wa mkoa wa Mara wasikitishwa na uongozi wa hifadhi ya Serengeti.
Wabunge wa mkoa wa Mara wameonesha kusikitishwa kwa kiasi kikubwa na kitendo cha uongozi wa hifadhi ya taifa ya Serengeti kushindwa kuchangia fedhwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya imaendeleo katika vijiji vinavyozunguka hifadhi hilo huku wakidai miradi hiyo imekuwa kutolewa kwa ubaguzi hatua ambayo wamesema imechangia kuongeza chuki kati ya wananchi na wahifadhi.
Wakizungumza katika kikao cha ushauri cha mkoa RCC mkoani Mara wabunge hao kwa umoja wao, wamesema licha ya eneo kubwa la hifadhi ya taifa ya Serengeti kuwa mkoa wa Mara, lakini wananchi wake wameshindwa kunufaika na hifadhi hiyo ukilinganisha na mikoa mingine.
Hata hivyo mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya Serengeti Bw William Mwakilema, akizungumza katika kikao hicho amesema hifadhi hiyo imekuwa ikichangia huduma za jamii katika vijiji vinavyozunguka hifadhi yake lakini pia kuchangia pato la taifa.
Wilaya za mkoa wa Mara zinazopakana na hifadhi hiyo ya taifa ya Serengeti ni pamoja wilaya ya Serengeti, Bunda na Tarime.
Post a Comment