Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

IZI NI KANUNI 30 KWA WANAWAKE WALIOPO KWENYE NDOA

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.

1). Usinyanyue sauti mbele ya mumeo kwa sababu yoyote ile. Hiyo ni ishara ya utovu wa heshima.

2). Usifichue udhaifu wa mumeo kwa familia na marafiki zako. Itakurudia. Wewe ni mlinzi wa mumeo, naye mumeo ni mlinzi wako.

3). Usitumie mihemko yako hasi kuwasiliana na mumeo, hujui namna mumeo atakavyoitafsiri. Wanawake  wenye hulka ya kujihami huwatengenezi nyumba yenye furaha hata siku moja.

4). Usimlinganishe mumeo na wanaume wengine, hujui maisha yao halisi yalivyo. Ukiibomoa hadhi yake, maana upendo wake kwako utashuka mara dufu.

5). Usiwatendee vibaya marafiki wa mumeo kwa sababu huwapendi, mtu anayetakiwa kuwa wa kwanza kujitenga nao ni mumeo.

6). Usisahau kuwa mumeo alikuoa, yeye si mfanyakazi wako au mtu mwingine tofauti. Tekeleza majukumu yako kama mke.

7). Usimpe mtu mwingine fursa ya kumhudumia mumeo, watu wanaweza kufanya mambo mengine, lakini huduma za mumeo ni jukumu lako mwenyewe.

8). Usimlaumu mumeo akija nyumbani mikono mitupu. Badala yake mpe nguvu, mhamasishe na umfariji.

9). Usiwe mke mwenye matumizi ya hovyo, jasho la mumeo halitakiwi kutumiwa hovyo.

10). Usijifanye kuwa mgonjwa kwa lengo la kumnyima tendo la ndoa. Mpe kwa namna apendavyo. Tendo la ndoa ni muhimu sana kwa wanaume, ukiendelea kumnyima haitachukua muda mrefu kabla mwanamke mwingine hajatimiza jukumu hilo. Hakuna mwanaume anayeweza kustahmili kukosa tendo la ndoa kwa muda mrefu.

11). Usimlinganishe mumeo na mwanaume wako wa zamani kitandani. Ukifanya hivyo, nyumba yako inaweza kupata mtikisiko wa aina yake.

12). Usijibishane na mumeo hadharani. Hilo litashusha hadhi na heshima yake. Hitaji namba moja la mwanaume ni heshima kwanza na sio kitu kingine.

13). Usimpe changamoto mumeo mbele ya watoto. Wanawake wenye busara hawafanyi hivyo.

14). Usisahau kumuandaa mumeo na kuhakikisha kuwa yuko maridadi kabla hajatoka nyumbani.

15). Usiruhusu marafiki zako kuwa karibu mno na mumeo.

                     Picha kutoka maktaba 

16). Usiwe na haraka unapokuwa bafuni na kwenye dressing table. Huko nje mumeo anakutana na wanawake ambao wanatumia muda wao kujiremba vizuri bila haraka yoyote ili waonekane maridhawa, jiandae taratiibu kabisa.

17). Wazazi au familia yako hawana umuhimu mkubwa katika ndoa yenu. Ila endelea kuwaheshimu, na uwashirikishe kwa raha na shida.

18). Usiegemeze upendo wako kwenye vitu vya pesa. Endelea kumheshimu mumeo kwa kila kitu anachokuwa amefanikiwa kupata kwa mda mlio weza kuishi pamoja.

19). Usisahau kuwa mume anahitaji mke mwenye umakini na mwenye usikivu mzuri, hivyo unapozungumza naye acha mambo mengine. Mawasiliano mazuri ndiyo msingi wa nyumba yenye furaha.

20). Iwapo mawazo yako yamefanikisha jambo kuliko mawazo yake, usijilinganishe naye. Bali ishini na mfanye kazi kama timu maana ndio wajibu wenu.

21). Usiwe msumbufu kwa mumeo. Hakuna mume anayependa mke msumbufu hata siku moja.

22). Mke mvivu hajali. Hata hajui kwamba anatakiwa kuoga na kuwa msafi. Zidisha usafi wa mwili pamoja na usafi wa akili.

23). Je, mumeo anapenda chakula fulani? Kuwa makini sana kwenye namna ya utayarishaji wa chakula. Hakuna mume anayefanya maskhara na suala la chakula.

24). Usiwe mtu wa kumkamua sana mumeo, ukataka kila kitu uwe nacho wewe. Furahia kile kinachopatikana kulingana na uwezo wake.

25). Ifanye glasi ya maji kuwa ukaribisho wa kwanza kwa mumeo na kwa kila mgeni anayeingia nyumbani kwenu. Ukarimu maridhawa ndiyo uzuri wa kweli.

26). Usijenge urafiki na wanawake wenye mtazamo hasi na wa kimakosa kuhusu ndoa, maana kuwa nao unaweza kuaribu ndoa yako kutokana na tabia zao.

27). Ndoa yako itakuwa na thamani kama utaipa thamani. Uzembe na kutojali ni sumu ya ndoa yako ilo litambue.

28). Watoto ni zawadi adhimu kutoka kwa Mungu, wapende na uwafunze mambo mazuri na yaliyo mema kwao pamoja na maisha yao kwa ujumla.

29). Umri usiwe kikwazo cha kuwa na ushawishi kwenye nyumba yako. Kamwe usipunguze kiwango cha huduma kwa familia yako kwa hali yoyote ile. Ifanye huduma yako kuwa yenye kujaa ubunifu maridhawa kila siku ya Mungu.

30). Mke anayemuabudu Mungu ni mke maridadi, daima muombee mumeo na familia yako kwa ujumla wake.

Ukiweza kuyafuata mambo yote haya 30 basi ndoa yako itakuwa imara siki zote. Na ukiyashindwa mambo haya 30 basi wewe ndoa huiwezi kabisa.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top