Habari za leo ndugu mdau wa Tazama Line, leo katika ukurasa wa kero yangu tujikite katika suala zima la mpangaji aliyepanga chumba kimoja/viwili au aliyepanga frem moja /mbili.
Tangu mwaka jana tatizo hili limekuwa kero kwa wapangaji wengi ambapo unakutana baada ya kuisha kwa mkataba wako wa pango pindi unapolipa tena kodi mpya iwe ni kodi ya miezi mitatu/miezi sita au mwaka mzima badala ya kupewa mkataba wako siku iyoiyo uliyotoa pesa ya kodi mpya unakuja kupewa mkataba wako zaidi ya siku nne/kumi/mwezi bila ya mmiriki wa kile ulichopanga kukuomba samahani kwa kuchelewesha mkataba wako.
Kiutaratibu unatakiwa pindi unapokuwa mezani wewe mpangaji pamoja na mpangishaji siku ya kulipa kodi mpya ni lazima na mikataba isahinishwe siku iyoiyo ya malipo na endapo kama haipo basi mpangishaji anatakiwa akuombe radhi kwa kutokuwepo kwa mikataba hiyo na akuaidi ni siku gani italetwa ili isahiniwe na kila mtu awe na mkataba wake.
Ili kuondoa usumbufu na ugomvi usio wa lazima wapangishaji/wamiriki wa nyumba/frem mnatakiwa kutoa mikataba ya wangaji wenu kwa wakati kama nyinyi mnavyodai kodi zenu kwa wakati.
Endapo mpangaji akichelewa kutoa pesa ya kodi siku moja tu waga mnakuwa wakali sana, sasa ili nawao wasiwe wakali kwenu basi timizeni vigezo na masharti ya kupangisha.
Wapangaji wanakutana na mambo mengi sana katika nyumba za kupanga ikiwemo manyanyaso, masengenyo nk, Poleni sana wapangaji, sasa unaweza kutuma kero yako kwanjia ya message au what's App kupitia 0659919292 nasi tutaifanyia kazi kero yako.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment