Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), linaendelea
kuitafakari Serikali ya Tanzania kuhusu kuingizwa katika mkataba wa pili
wa miradi ya shirika hilo. Msemaji wa Ubalozi wa Marekani nchini, Marissa Maurer, aliliambia
Nipashe kuwa hivi sasa mchakato wa maandalizi ya mkataba wa pili wa MCC
na Tanzania unaendelea.
Hata hivyo, alisema mkataba huo hautawasilishwa mbele ya Bodi ya MCC ili kuidhinishwa hadi maandalizi yake yatakapokamilika.
Alisema mkataba huo pia hautaweza kuidhinishwa hadi pale Tanzania
itakapoonyesha hatua ilizopiga katika mageuzi ya uchumi katika sekta ya
nishati kama ilivyoahidi kufanya hivyo hadi mwishoni mwa mwaka jana.
Desemba mwaka jana, ubalozi huo ulitoa taarifa kwa vyombo vya habari
kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya MCC ilikutana Desemba 10, mwaka huo katika
mkutano wake wa kila mwaka wa kuchagua nchi zitazopatiwa fedha na
shirika hilo. Katika mkutano huo, bodi hiyo ilipiga kura ya kuiruhusu Tanzania
iendelee na maandalizi kwa ajili ya mkataba wa pili wa miradi ya MCC.
Aidha, bodi hiyo iliihimiza Serikali ya Tanzania kuchukua hatua
thabiti za kukabiliana na rushwa kama sharti la msingi kwa MCC kufanya
maamuzi ya mwisho ya kuidhinisha mkataba huo.
Kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 200 katika akaunti ya
Tegeta Escrow katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kilikuwa kikwazo
kingine kwa shirika hilo kuiingiza Tanzania katika mkataba huo hadi
litakaporidhishwa na hatua ambazo zingechukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa
kashfa hiyo.
Nchi ambazo zimekuwa zikiingizwa katika mikataba ya miradi ya shirika
hilo, zimekuwa zikipewa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment