Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi, Andrew Chenge
leo atapandishwa kizimbani kuhojiwa na Baraza la Maadili ya Viongozi wa
Umma kwa kuhusika katika kashfa ya ‘kuchota’ fedha kwenye Akaunti ya
Tegeta Escrow.
Chenge ni mmoja wa viongozi waliopata mgawo wa fedha kutoka kwenye
akaunti hiyo jambo ambalo ni ukiukaji wa sheria namba 13 ya maadili ya
viongozi wa umma.
Watuhumiwa wengine ni aliyekuwa waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, mkurugenzi wa sheria, Wizara ya Ardhi, Rugonzibwa Mujunangoma na Mnikulu wa Ikulu, Shaaban Gurumo.
Chenge alifungua kesi Mahakama Kuu akipinga kuhojiwa dhidi ya tuhuma
za kukiuka maadili ya viongozi baada ya kupokea Sh1.6 bilioni kutoka kwa
mkurugenzi wa VIP Engineering, James Rugemalira, fedha ambazo
zinahusishwa na akaunti hiyo.
Katika vikao vilivyopita, Chenge alilitaka baraza kutojadili shauri
lake kwa sababu kesi yake ya msingi kuhusu fedha za escrow ilikuwa
imefunguliwa Mahakama Kuu.
Kashfa ya escrow ilisababisha aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo na waziri wa Ardhi, Profesa Tibaijuka
kuondolewa katika nyadhifa zao.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment