Mayai ni miongoni mwa chakula ambacho wengi hukitumia kama kibururdisho tu mara nyingi, lakini kimsingi mayai yanaumuhimu wake pia kwa afya hasa unapopata yale ya kienyeji.
Vifuatavyo ni virutubisho muhimu ambavyo hupatikana ndani ya mayai
Mayai ni chanzo kizuri cha protini ya kutosha, ambayo husaidia sana kujenga misuli, ngozi na homoni za mwilini.
Mayi yana vitamini D, ambayo humarisha afya ya mifupa pamoja na meno, lakini pia ina vitamin B 2., B 6 pamoja na vitamin B12.
Aidha, mayai yana madini ya chuma, copper pamoja na zinc ambayo kwa pamoja hushirikiana kuimarisha afya ya mwili.
Pia mayai yana vitamin A, na vitamin K
Zifuatazo ni aina ya virutubisho vinavyopatikana kwenye mayai na asilimi yake kwa ujumla.
Vitamin A: 6%
Folate: 5%
Vitamin B5: 7%
Vitamin B12: 9%
Vitamin B2: 15%
Phosphorus: 9%
Selenium: 22%
Post a Comment