Hivi ni mara ngapi unajikuta tumbo limejaa gesi na usijue nini cha kufanya? inawezekana hiyo hali imekuwa ikikukuta mara kadhaa na ukashindwa kujua jambo gani ufanye.
Lakini fahamu kwamba hali ya tumbo kujaa gesi huweza kusababishwa na kumeza kwa kiasi cha hewa wakati wa kumeza chakula au kunywa vinywaji mbalimbali.
Sasa leo napenda kukwambia ukikutwa na hali hiyo unaweza kujitahidi kujaribu kufanya haya yafuuatayo:
Kula matunda yenye majimaji mengi kwa wingi mfano tikiti maji, mapapi ambayo husaidia sana kurahisha usagaji wa chakula tumboni.
Aidha, unaweza kujitahidi kunywa maji mengi angalau ufikishe lita 3 hadi 4 kwa siku ambayo yatakusaidia sana kuondokana na tatizo hilo.
Pia unaweza kula mlo mdogo mdogo, lakini mara kwa mara na kujiepusha na vyakula na vinywaji vyenye gesi.
Lakini kama hali inaendelea unaweza kufika kwenye kituo cha afya kilicho karibu kwa uchunguzi zaidi.
Post a Comment