KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye
amepata ajali mbaya jana usiku akiwa njiani kuelekea Lindi akitokea
jijini Dar es Salaam.
Nape ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la
Mtama, Lindi alipata ajali hiyo baada ya tairi la mbele la gari
aliyokuwa akiendesha aina ya Toyota Land Cruiser kupasuka na kupinduka
mara kadhaa katika eneo la Nyangao mkoani Lindi.
Katika gari hilo, Nape alikuwa peke yake na ndiye alikuwa akiendesha gari hilo ambapo amepata majeraha madogo ila anaendelea vizuri.
Akizungumza na mtandao huu, Nape amesema: “Namshukuru Mungu nimetoka salama na nawaomba wananchi wasiwe na hofu japo ajali ilikuwa mbaya maana gari lilipinduka mara kadhaa, nimepata majeraha madogomadogo na michubuko ila ni mzima.
Gari limeharibika vibaya ila ninachoshukuru nilikuwa nimefunga mkanda na ‘air bag’ nazo zimenisaidia.”
Kabla
ya ajali hiyo, Nape alikuwa jijini Dar es Salaam ambapo aliungana na
mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli aliyekuwa na
mikutano kadhaa ya kampeni katika jiji la Dar na baada ya shughuli hiyo
alikuwa akirejea Lindi kuendelea na kampeni kwenye jimbo lake la Mtama.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment