Wanafunzi kumi na moja wa shule za msingi zilizopo wilayani hapa Mkoa wa Pwani wamedaiwa
Wanafunzi wa moja ya shule za msingi nchini. Picha kwa msaada wa mtandao.
Kibaha. Wanafunzi kumi na moja wa shule za msingi zilizopo wilayani hapa Mkoa wa Pwani wamedaiwa kulawitiwa na kuambukizwa magonjwa ya zinaa.
Mjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa Mtoto ambaye pia ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mwendapole, Shabani Ditesua alisema jana kuwa hadi sasa, wamepokea mashauri 11 ya wanafunzi kufanyiwa vitendo hivyo vya kinyama.
Ditesua alisema hayo katika kikao cha kamati hiyo kilichoandaliwa na Mradi wa Kupinga Ukatili dhidi ya watoto ulio chini ya Shirika la Plan International.
Ditesua alisema waliamua kupeleka taarifa hizo polisi, lakini kuna wazazi waliomba kesi zifutwe ili kuondoa aibu kwa watoto wao.
Ditesua alisema kati ya watoto hao, wako waliofanyiwa vitendo hivyo kinyume na maumbile na baadhi kunajisiwa na wanaume wenye umri mkubwa.
Alisema mbali na kufanyiwa vitendo hivyo na wakubwa, baadhi ya wanafunzi hujamiina wenyewe wanapokuwa shuleni.
Ditesua alisema waliogundulika kuwa na mchezo huo kwa wenzao wamehamishiwa shule nyingine ili kupunguza athari ya kuathirika kisaikolojia kwa waliofanyiwa vitendo hivyo.
Mjumbe huyo aliitaka Serikali kuhakikisha inachukua hatua za haraka ili kuwanusuru wanafunzi kufanyiwa vitendo hivyo.
Post a Comment